Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Vikosi vya serikali ya Syria vikisaidiwa na ndege za kivita za Urusi na kuongozwa na wataalamu wa vita kutoka Iran ambao wanaongoza majeshi ya nchi kavu, vimeingia katika mji wa kale wa Palmyra ulitekwa na Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani tokea mwezi wa Mei mwaka 2015 .
Wakati hayo yanaendelea serikali ya Iraqimeanza operesheni ya kijeshi iliokuwa ikusubiriwa kwa muda mrefu ya kuukombowa mji kaskazini wa Mosul nchini humo na mpaka sasa wamefanikiwa kukomboa vijiji vinane kutoka mikono ya magaidi wa Daesh wanaungwa mkono na Saudia arabia na washirika wake.
Kusonga mbele kwa majeshi ya Syria kwenye mji wa Palmyra ambao ni turathi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) baada ya vikosi hivyo vya serikali kuweza kuteka milima kadhaa na maeneo ya nyanda za juu karibu na mji huo unaojulikana kwa machimbo yake ya kale yasiothaminika na mabaki ya Waroma. Vikosi vya Syria vimekuwa vikishambulia mji huo kwa siku kadhaa katika juhudi za kuukombowa mji huo kutoka katika mikono michafu ya magaidi wanaoungwa mkono na Marekani, na mpaka sasa majeshi ya Syria yamesha ukomboa mji huo kwa asilimia 70.
Mwisho wa habari/ 291