Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mtu mmoja amekufa na wengine kadhaa wakiwemo watoto wamejeruhiwa baada ya maeneo kadhaa ya Ulaya likiwemo la bustani mjini Paris na uwanja mmoja wa soka nchini Ujerumani kupigwa na radi hapo jana. Nchini Poland vyombo vya habari vimeripoti kuwa mtu mmoja aliuwawa na radi pale alipokuwa akishuka katika mlima wa Babia Gora. Kwa Ujerumani zaidi ya watu 30 walipelekwa hosipitali katika kijiji cha magharibi cha Hoppstaedten pale ambapo radi ilipopiga katika kiwanja cha soka mwishoni mwa mechi ya watoto. Watu wazima watatu wamejeruhuiwa vibaya sana akiwemo mwamuzi wa mchezo watoto wengi wenye umri kati ya miaka saba na minane pia wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali kama tahadhari.
Mwisho wa habari/ 291