Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri mkuu wa Iraq ameonyesha matumaini kwamba mwaka huu wa Kiislamu tutapata ushindi mkubwa dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh na kuzikomboa sehemu zote ziliobaki chini ya kikundi hicho cha kigaidi.
Hayo yamesemwa na Haider al-Abadi (waziri mkuu wa Iraq) katika maelezo yake na akisisitiza kuwa: matumaini yetu ni kwamba mwaka mpya wa Kiislamu ni mwaka wa ushindi mkubwa dhidi ya Daesh ambapo tutazikomboa sehemu zote zinazokaliwa na magaidi, hususan mji wa Musol ambao uko chini ya kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Aidha amebainisha kuwa viongozi wa Iraq wako wanasubiri kwa hamu kuanza mashambulizi ya kuikomboa wilaya ya Musol nchini humo.
Waziri mkuu wa Iraq amesema katika kongamano la kielimu katika makao makuu ya uhakiki wa kitaifa wizara ya kazi na mambo ya kijamii amebainisha kuwa: tutaendeleza vita dhidi ya magaidi nchini Iraq na kufanya juhudi za kusambaratisha sababu za kuwepo magaidi hao.
Alimalizia kusema kuwa: magaidi hutumia fursa mbalimbali za kuwateka wananchi ikiwemo umasikini na ufakiri, hivyo tunapaswa kufanya juhudi za makusudi za kukabiliana na hali hiyo, lakini pamoja na kuwepo vikwazo vingi nchini Iraq mpaka sasa imefanikiwa kupata ushindi mkubwa dhidi ya kikundi hicho.
mwisho wa Habari/290
2 Oktoba 2016 - 20:54
Msimbo wa Habari: 782915
Waziri mkuu wa Iraq ameashiria hasara kubwa ilioingizwa na vikundi vya kigaidi nchini humo nakusema kuwa: vikundi vya kigaidi nchini Iraq vimeisababishia hasara ya dola bilioni 35 nchini hiyo