Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mashambulio ya anga ya majeshi ya Serikali yanayoendelea Syria, yamewaua magaidi wanaodhaminiwa na Marekani wasiopungua 20 katika mji wa Aleppo.
Wakati huo huo, makombora yaliyoyoilenga shule moja ambayo ni ngome ya magiadi kusini mwa Syria yameua magaidi sita, wakiwemo watoto kadhaa. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa wanaharakati na vituo vya habari vya serikali ya Syria. Mji wa Aleppo uliopo Syria ya kaskazini umekuwa ukishuhudia mapigano makali katika miezi iliyopita. Majeshi ya serikali na washirika wake yanajaribu kuyateka maeneo yanayoshikiliwa na magiadi wanaoupinga utawala wa Rais Bashar al Assad na kupewa silaha na Marekai. Wakati huo huo, Syria inamlaumu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-Moon, kwa kuegemea upande mmoja katika migogoro ya kimataifa. Chanzo kimoja kutoka wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo kimesema Ban ameiharibu sifa ya kuaminika kwa Umoja wa Mataifa.
Mwisho wa habari/ 291