27 Oktoba 2016 - 18:41
Mgogoro wa Syria wazua malumbano Umoja wa Mataifa

Wakati mamilioni ya wananchi wa Yemen wakitaabika kwa mashambilizi makali yanayofanywa na Saudia arabia ikishirikiana na Marekani, Ufaransa, Uingereza na Israel, kwa madai ya kumrudisha madarakani Rais Haadi anayepingwa na wananchi, baadhi ya makada wa Umoja wa mataifa wameshangaza ulimwengu baada ya kulailaumu Urusi kwa kuwashambulia magaidi nchini Syria.

Shirika la habari la ABNA linarioti kuwa: Wakati mamilioni ya wananchi wa Yemen wakitaabika kwa mashambilizi makali yanayofanywa na Saudia arabia ikishirikiana na Marekani, Ufaransa, Uingereza na Israel, kwa madai ya kumrudisha madarakani Rais Haadi anayepingwa na wananchi, baadhi ya makada wa Umoja wa mataifa wameshangaza ulimwengu baada ya kulailaumu Urusi kwa kuwashambulia magaidi nchini Syria.

Naibu katibu mkuu wa UN wa kitengo cha misaada ya kibinadamu ameilaumu Urusi na Syria kwa kutumia mabomu dhidi ya magaidi mjini Aleppo kuwashinikiza magaidi kujisalimisha, jambo lililozua majibizano makali na Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa.

Majibizano hayo yalizuka baada ya naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia misaada ya kibinadamu Stephen O´brien kulihutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu kile alichokitaja kuwa hali ya kuogofya katika eneo linalodhibitiwa na magaidi la Mashariki mwa Aleppo ambapo magaidi wanaoungwa mkono na Marekani zaidi ya 400 wameuawa na takriban wngine zaidi ya elfu moja kujeruhiwa katika muda wa chini ya mwezi mmoja .

O'Brien aliilaumu Syria kwa kuuzingira mji huo wa magaidi na wakati huo huo kufanya kampeini ya mashambulizi ya mabomu pamoja na washirika wake wa Urusi katika kampeini ya maksudi ya kufanya maisha ya wakazi wa eneo hilo kuwa magumu zaidi.

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa ambaye pia ni rais wa sasa wa Baraza la Usalama la Umoja huo Vitaly Churkin alijibu akisema tuhuma hizo ni za kushangaza sana.

Churkin ameongeza   kwamba O’Brien alizungumzia kuhusu mabomu hayo kama yanayorushwa hivi sasa katika eneo la Mashariki mwa Aleppo ambalo ni ngome ya magaidi wanaoungwa mkono na Marekani, wakati mashambulizi hayo yalisitishwa kwa siku saba sasa na pia kuleta dhana kwamba silaha za kemikali zimekuwa zikutumiwa katika mji huo .

Alitaka kutolewe ushahidi na kumlaumu O’Brien kwa kushindwa kutaja kuwa ngome ya serikali ya eneo la Magharibi mwa Aleppo limekuwa chini ya kundi la magaidi la al- nusra lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida ambayo yote yanaungwa mkono na Marekani na washirika wake nchini Syria.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power aliongezea sauti yake katika kuishutumu Urusi na kusisitiza kuwa ilihusika katika mashambulizi hayo kwa kutumia silaha ambazo hazijawahi kutumiwa hata katika uongozi wa kidemokrasia nchini Syria.

Stephen O’Brien alitoa wito kwa pande zote husika zinazotatiza usaidizi kufika katika eneo la Mashariki mwa Aleppo na mbinu mbali mbali za mateso kusitisha hatua hizo na kuruhusu maelfu ya watu waliokwama kwa kutekwa na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani katika maeneo mengine 17 nchini humo kupata usaidizi. Marekani, Uingereza na Ufaransa zilimuunga zinaunga mkono magaidi nchini Syria na kusababisha vifo vya maelfu ya watu wasio na hatia.

Mwisho wa habari/ 291