27 Oktoba 2016 - 18:46
Magaidi wa Daesh zaidi ya  100  wameuawa Iraq

...Viongozi wa Iraq wanazilaumu Marekani na Uturuki kwa kuwatorosha mamia ya magaidi wa Daesh na kuwafungulia njia ya kuelekea nchini Syria.

Shirika la habari la ABNA linarioti kuwa: Zaidi ya wapiganaji 1000 wa  kundi la kigaidi la Daesh linalofahamika kama Dola la Kiislamu, wameuawa katika mashambulizi ya kuukomboa mji wa Mosul nchini Iraq, wakati kambi karibu na mji huo zikifurika raia wanaokimbia mapigano. Operesheni hiyo iliyoanzishwa Oktoba 17, imeshuhudia maelfu ya wanajeshi wa Iraq wakiongozwa na wataalamu wa vita kutoka Iran wakiisogelea Mosul kutokea kusini, mashariki na kaskazini katika jaribio la kuukomboa mji huo muhimu wa mwisho wa Iraq ulio chini ya udhibiti wa magaidi wa Daesh walio na ukaribu na Uturuki na Marekani.

 Viongozi wa Iraq wanazilaumu Marekani na Uturuki kwa kuwatorosha mamia ya magaidi wa Daesh na kuwafungulia njia ya kuelekea nchini Syria.

Wakati hayo yanaendelea Jeshi la Urusi limeshambulia magaidi zaidi ya 200 ya wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi waliopewa upenyo wa kutoroka na Marekani kuelekea Syria, ambako Marekani na washirika wake kutoka nchi 61 wanalengo la kuiangusha serikali halali ya Bashar asad.

Mwisho wa habari/ 291