Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Ufaransa ambayo ni miongoni mwa wadhamini kubwa wa magaidi wanaoitwa kuwa ni magaidi wa msimamo wa kati wasio na madhara, imeitisha kikao cha kutaka kuishinikiza serikali ya Syria na washika wake waache kuwashambulia magaidi wanaoleta uharibifu mkubwa nchini humo, na badala yake kuzungumza nao na kugawana madaraka.
Mkutano huo kushinikiza vikwazo zaidi kuwekewa serikali ya Syria ili ikose nguvu ya kupambana na magaidi.
Takriban familia 100 zilizojaribu kutoroka kutoka mji wa Allepo ambao uko mikononi mwa magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na Ufaransa, zililazimika kurudi kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na magaidi hao hatari.
Ufaransa sasa imeitisha mkutano wa nchi ambazo zinaunga mkono magaidi nchini Syria ikiwemo Marekani na mataifa ya ghuba kujadili hali ilivyo nchini humo hasa mashambulizi dhidi ya mji wa Aleppo. Hayo yanajiri wakati mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura akihofia huenda rais Bashar al-Assad akafanya shambulizi zaidi dhidi ya magaidi kabla rais mteule Donald Trump kuapishwa.
Waziri wa mambo ya nje ya Ufaransa Jean-Marc Ayrault amesema mkutano huo wa nchi ambazo ni marafiki wa magaidi nchini Syria utafanyika mjini Paris mapema mwezi Disemba. Amesisitiza kuwa jumuiya za kimataifa lazima zikome kuangalia tu uhalisia mchungu unaoendelea nchini Syria hasa mji unaoshambuliwa wa Aleppo.
Nchi ambazo zimealikwa ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Italia, Uingereza na Uturuki, kando na mataifa ya ghuba hasa Saudi Arabia, Qatar, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu ambazo zote zinaunga mkono upande wa magaidi nchini Syria na kukabiliana na serikali ya Syria inayoungwa mkono na Urusi na Iran.
Jean Marc Ayrault anasema "Leo, karibu watu milioni moja wamezingirwa katika mashambulio kulingana na Umoja wa Mataifa, sit u Aleppo wala Homs lakini pia Ghouta na Idlib. Huo ndio uhalisia wa Syria kwa sasa. Ufaransa inachukua hatuaya mkutano kukabili mkakati huo wa vita unaofanywa na serikali na washirika wake ambao wamechukua nafasi ya ukosefu wa uhakika wa Marekani katika kusaidia magaidi baada ya rais mtarajiwa Trump kupinga serikali yake kusaidia magaidi nchini Syria na Iraq. Pia tutajadili msimamo wa Umoja wa Mataifa wa kukemea matumizi ya zana za kemikali na serikali ya Syria."
Raia washindwa kutoka maeneo ya vita
Takriban familia mia moja zilizojaribu kuhama mji huo usiku wa jana, zililazimika kurudi kufuatia mashambulizi makali yaliyofanywa na magaidi dhidi yao. hayo yamesemwa na kundi moja la uchunguzi. Serikali imeimarisha mashambulio kudhibiti mashariki ya mji huo ambao ni ngome kuu iliyosalia ya magaidi hao, jambo linalowapa hofu wadhamini wa magaidi hao, serikali ya inawalaumu magaidi kwa kuzuia raia wasitoke na kuwatumia kama ngao, wiki iliyopita takriban raia 30 waliuawa na magaidi hao baada ya kufanya maandamano ya kutaka waruhusiwe kutoka mikononi mwa magaidi hao.
Vikosi vya serikali ya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi vimeendeleza mashambulizi makali dhidi ya magaidi katika mji wa Aleppo kuukumboa kutoka mikononi mwa magidi hao hatari, ambao Marekani na washirika wake wanaita kuwa ni magaidi wasio na madhara. Inakadiriwa kuwa raia 140 wamefariki katika kipindi cha wiki moja iliyopita kufuatia mashambulizi yanayofanywa na magaidi hao.
Hofu ya mashambulio zaidi
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura ambaye anatuhumiwa kwa kupendelea magaidi amesema anayo hofu kwamba huenda rais Bashar al-Assad akafanya mashambulio mapya mashariki mwa Aleppo dhidi ya magaidi kabla ya rais mteule Donald Trump kuapishwa tarehe 20 Januari.
Japo de Mistura hajaelezea sababu ya hofu yake, wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema ushindi wa Trump umempa Assad matumaini ya ushirikiano na mshirika wake Urusi dhidi ya magaidi ambao wanapata msaada kutoka serikali ya Obama, huku vyombo vya habari vikubwa duniani vikiendelea kutangaza habari kuwa serikali ya Syria inaua raia, huku vyombo hivyo vya habari vikijizuia kutangaza mauaji ya kinyama yanayofanywa na Saudia arabia na washirika wake nchini Yemen, kwa zaidi ya mwaka mmoja huku wakiwa wamezuia hata chakula na madawa yasiwafikie wananchi wa Yemen.
Mwisho wa habari/ 291