Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wametangaza kuwa watatuma vikosi vya kijeshi nchini Gambia, iwapo kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Rais Yahya Jammeh, atakataa kuachia madaraka mwezi ujao. Uamuzi huo ulitangazwa na rais wa Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Marcel de Souza, hapo jana. Souza amewaambia maripota kuwa jumuiya hiyo imeiteua Senegal kuongoza ujumbe huo wa kijeshi. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa jumuiya ya mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS kuingilia mgogoro wa kikanda. Muungano wa upinzani umeapa kuhakikisha kuwa rais mteule Adama Barrow anaapishwa Januari, licha ya Rais Jammeh kutishia kubakia madarakani iwapo mahakama ya juu kabisa haitamuamuru kuondoka. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limevitolea wito vikosi vya Gambia kujizuia kutumia nguvu na kumtaka Jammeh akubali kushindwa.
Mwisho wa habar / 291