29 Desemba 2016 - 19:41
 Wapinzani wa serikali waunga mkono usitishaji mapigano Syria

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan leo amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin yaliyojikita juu ya hatua ya usitishaji mapigano nchini Syria inayotarajiwa kuanza usiku wa manane hii leo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan leo amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin yaliyojikita juu ya hatua ya usitishaji mapigano nchini Syria inayotarajiwa kuanza usiku wa manane hii leo. Msemaji wa Rais Erdogan amethibitisha katika taarifa yake. Viongozi hao pia walijadili juu ya mazungumzo kuhusu Syria yanayotarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Kazakhstan, Astana. Rais Putin alitangaza hatua ya kusitisha mapigano kati ya makundi ya upinzani na majeshi ya serikali ya Syria inayoanza baadaye leo. Taarifa hiyo ya Urusi inakuja baada ya Urusi, Iran na Uturuki kusema ziko tayari kufikia makubaliano ya amani kuhusu mgogoro wa Syria uliochukua karibu miaka sita sasa.

Muungano wa makundi ya upinzani nchini Syria unaunga mkono makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwataka wapiganaji wa makundi ya waasi kuheshimu hatua ya kusitisha mapigano katika nchi nzima. Samir Nashar ambaye ni mwanachama wa muungano wa makundi hayo unaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi amelieleza shirika la habari la Dpa kuwa muungano huo unatoa mwito kwa makundi kadhaa ya upinzani kutekeleza makubaliano ya usitishaji mapigano

Iran na washirika wake wa kundi la Hizbollah la Lebanon wanaiunga mkono serikali ya Syria katika kupambana na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani ikishirikiana na nchi 61 katika mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano. Msemaji wa muungano huo amesema jeshi la muungano wa makundi hayo ya upinzani litaheshimu makubaliano hayo ya kusitisha mapigano lakini litakuwa tayari kulipiza kisasi endapo makubaliano hayo yatavunjwa.

Mwisho wa habari/ 291