8 Januari 2017 - 10:54
Magaidi wawili wauliwa chini Saudi Arabia

Utawala wa Saudi Arabia umedai kuwaangamiza magaidi wawili hatari katika sehemu ya Yasmin katika mji mkuu wa nchi hiyo “Riyadh”

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya mambo ya ndani ya utawala wa Saudi Arabia umetangaza kuwa: katika mashambulizi ya vyombo vya usalama yaliofanyika mjini Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia wamefanikiwa kuuwa magaidi hatari wawili nchini humo.
Shambulio hilo limefanywa siku ya Jumamosi katika sehemu ya Yasmin kaskazni mwa mji wa Riyadh, ambapo kufuatia shambulio hilo mwanajeshi mmoja wa Saudi Arabia amejeruhiwa katika tukio hilo. Kwa mujibu wa ripoti hii kuwa magaidi hao wawili waliokuwa na majina ya “Talii Salim Sairiy” na “Talali Samran Said” wote wawili wananchi wa Saudi Arabia.
Shirika la habari la Saudi Arabia wametangaza kuwa Talii Sairiy ni mtaalamu wa masuala ya kutengeza mabomu ya mikanda kwaajili ya miripuko ya kigaidi nchii humo.
Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa, majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo baada ya kuwachunguza kwa muda mrefu na kuwaingiza katika mitego yao, katika sehemu wanayoishi magaidi hao sehemu ya Yasmin hatimaye kuwazingira, ama magaidi hao hawakutaka kujisalimisha ndipo yakaanza mapambano baina yao na majeshi ya nchi hiyo.
Aidha kwa mujibu wa maelezo ya msemaji mkuu huyo ni kwamba, wamekuta makanda miwili ya mabomu na bomulingine moja la kutengeza kwa mikono.
Vyombo vya habari vya serikali ya Saudi Arabia vimetangaza kuwa miezi kadhaa iliopita kulitokea mapigano ya kurushiana risasi baina ya majeshi ya nchi hiyo magaidi Daesh waliopo sehemu ya Humeh, sehemu moja iliopo katika mji wa Makka.

mwisho wa habari/290