Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwa uchache watu 20 wameuwawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa kufuatia mripuko wa kigadi uliotokea katika soko la matunda katika mji wa Parachinar nchini Pakistan.
Mripuko huo umetokea asubuhi ya leo katika soko hilo, ambapo mbunge wa jimbo la Parachina katika bunge la Pakistan amesema kuwaambia waandishi wa habari kuwa; kufuatia mripuko huo watu 20 wameuwawa na wengine 50 wajeruhiwa vibaya, huku akisisitiza kuwa watu 10 kati ya majeruhi hao, wako na hali mbaya.
Vyombo vya uokozi vilifika katika sehemu ya tukio hilo na kuwaamisha waathirika wa tukio hilo kwenda katika hospitali kuu ziliopo katika mji wa Parachinar.
Wasimamizi wa hospitali kuu za Parachinar wametangaza kuwa, mpaka sasa miili ya watu 5 miungoni mwa waliouwawa katika mripuko huo imewasilishwa katika hospitali hiyo.
Wasimamizi wa hospitali hiyo wameongeza kusema kuwa: kutokana na uchache wa vifaa na madaktari wazoefu, kuna uwezekano mkubwa wa kuwahamisha majeruhi hao kwenda katika hospitali kubwa za miji mingine nchini humo, kama vile hospitali ya mji wa Peshawar na Kohat.
Jeshi la Polisi la mji wa Parachinar wametangaza kwakusema kuwa mpaka sasa haijafahamika mripuko huo umetokea kwa mtu kujiripua au kwa kutega bomu na kuripua kwakutumia rimoti.
Walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa mripuko huo ni kujiripua ambapo mmoja kati ya magaidi alijiripua akiwa baina ya watu.
Muhammad Nawazi Sharif ambaye ni waziri mkuu wa nchi hiyo, Asif Ali Zardari aliyekuwa Rais wa amani wa nchi hiyo na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo wametoa ujumbe wa kulaani tukio hilo la kigaidi, huku wakitoa rambirambi kwa familia ya waliouwawa kufuatia tukio hilo na kuwataka wauguzi na madaktari kutoa huduma nzuri kwa waathirika.
Mpaka sasa hakuna kikundi chochote kilichojihusisha na kufanya tukio hilo.
Ripoti zinaonyesha kuwa hii ni mara ya pili katika miezi ya havi mwishoni ambapo soko la matunda la mji wa Parachinar nchini Pakistan. 










mwisho wa habari/290