Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Marekani Donald Trump ameutetea uamuzi wake uliokosolewa vikali wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Syria, wakati wa ziara ya ghafla nchini Iraq ambayo. Rais huyo wa Marekani aliyeandamana na mkewe Melania, aliwaambia wanajeshi wa Marekani wakati wa ziara yake ya masaa matatu katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Al Asad, kuwa Marekani haiwezi kuendelea kuwa polisi ya ulimwengu, bali wanataka kuilinda nchi yao. Alisema kundi linalojiita Daesh au Dola la Kiislamu - IS limetokomezwa karibu lote na kuwa kituo hicho cha Iraq bado kitaendelea kutumika kupambana na kundi la kigaidi la Daesh. Ziara hiyo, ya kwanza ya Trump katika eneo la vita tangu alipochukua madaraka - imekuja wakati kukiwa na wasiwasi kuhusu sera ya Trump katika Mashariki ya Kati baada ya kutangaza kujiondoa Syria na kupunguza wanajeshi wake nchini Afghanistan. Trump hakukutana na maafisa wowote wa Iraq wakati wa ziara hiyo, lakini alizungumza kwenye simu na Waziri Mkuu wa Iraq Adel Abdul-Mahdi.
Kuondoka kwa Marekani nchini Syria kutapelekea nchi hiyo kumaliza migogoro yake kwa amani, nchi nyingi zinataman Marekani iondoke kabisa katika mashariki yakati.
Mwisho wa habari / 291