9 Januari 2019 - 09:02
  Iran yavikosoa vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi yake

Iran imekuwa ikiandamwa na vikwazo mbalimbali kwa kipindi cha miaka 40 sasa, na hii inatokana na nchi hiyo ya kiislamu kukataa kabisa kuwa chini ya nchi za magharibi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif amesema vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya nchi hiyo, haviondoi shaka kwamba Ulaya inahusika na kuwahifadhi magaidi. Jana Umoja wa Ulaya uliiwekea Iran vikwazo kwa kuhusika na mauaji ya wapinzani wake wawili katika ardhi ya Uholanzi pamoja na kujaribu kufanya mashambulizi dhidi ya wapinzani kwenye nchi za Ufaransa na Denmark. Umoja huo umezuia mali za idara ya ujasusi ya Iran pamoja na wafanyakazi wake wawili. Vikwazo hivyo vinahusu pia marufuku ya kusafiri. Zarif ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba mataifa ya Ulaya, ikiwemo Denmark, Uholanzi na Ufaransa yanawahifadhi wafuasi wa kundi la upinzani la Mujahedeen-e Khalq, MEK ambao wanaishi uhamishoni.

Iran imekuwa ikiandamwa na vikwazo mbalimbali kwa kipindi cha miaka 40 sasa, na hii inatokana na nchi hiyo ya kiislamu kukataa kabisa kuwa chini ya nchi za magharibi.

Mwisho wa habari / 291