9 Januari 2019 - 17:57
Kambi ya magaidi yasambaratishwa nchini Morocco

Wizara ya mambo ya ndani nchini Morocco imetangaza kuisambaratisha kambi moja ya magaidi wanaoshikamana na magaidi wa Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na wizara ya mambo ya ndani ya Morocco na kubainisha kuwa wizara hiyo imefanikiwa kikisambaratisha kikundi cha kigaidi kiliokuwa na fungamano na magaidi wa Daesh waliokuwepo katika miji mitatu nchini humo.
Katika kauli ya wizara hiyo imebainishwa kwamba vyombo vya usalama vya wizara hiyo kupata silaha baridi kutoka kwa watuhumiwa hao na kuwakuta na mabango ya kuwataka watu kuungana na kikundi hicho katika kufanya vitendo vya kigaidi, hali ambayo inaonyesha fungamano la watuhumiwa hao na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Pia watuhumiwa hao wamekutwa na kiasi kikubwa cha vifaa vinavyosababisha mripoko na nyaya za umeme zinazotumika kwa kufanya matukio ya kigaidi, huku wizara ikibainisha kuwa magaidi walikuwa katika mpango wa kufanya matukio ya kigaidi nchini humo ambapo walikuwa katika hali ya kupata mafunzo ya kujifunza kutengeza miripoko nchini humo.
Kukamatwa kwa magaidi hao kumetokea baada ya kuuwawa kwa mtalii mmoja aliouliwa kifo kibaya na magaidi wiki moja iliopita.
mwisho/290