12 Januari 2019 - 17:35
Magaidi 6 wauliwa kusini mwa Misri

Watu 6 miongoni mwa magaidi wauwawa baada ya kupambana na kurushiana risasi na majeshi ya usalama kusini mwa Misri

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya mambo ya ndani ya Misri leo imetangaza kuwasambaratisha magaidi 6  baada ya kurushiana risasi kwa muda na majeshi ya usalama wa nchi hiyo.
Katika kauli ya wizara hiyo imeeleza kuwa, vyombo vya ulinzi na usala vya wizara hiyo viligundua maficho ya magaidi hao ambapo leo walivamia na kuwashambulia na baada ya muda mrefu wa kujibishana kwa risasi, majeshi ya nchi hiyo yamefanikiwa kuwaangamia magaidi 6 kusini mwa Misri. Ama wizara hiyo mpaka sasa haijatoa maelezo kamili kuhusu tukio hilo.
mwisho/290