Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: amesema msaidizi wa masuala ya tamaduni katika Taasisi ya Hashdu Shaabiy alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya miaka arubaini ya mapinduzi ya kiislamu ya Iran maadhimisho ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Tamaduni ya Shahid Muhammad Baqir Sadr katika mji mtukufu wa Karbala ambapo alisisitiza kuwa: Trump anapaswa kufahamu kuwa Iraq ni moja ya sehemu ya viota vya mapambano dhidi ya ukandamizaji katika ukanda wa mashariki ya kati.
“Sayyed Hashim Alhaidariy” ameongeza kusema kuwa kama ilivyokuwa wazi kwamba serikali, wananchi na vikundi vyao vyote vya mapambano nchini Iraq viko pamoja vikitoa ujumbe mkali dhidi ya maneno machafu alioyatoa Trump kwamba “majeshi ya Marekani yataendelea kubaki nchini Iraq kwaajili ya kuichunguza na kuidhibiti Iran” hivyo wamarekani wanapaswa kufahamu kuwa hawana nafasi katika taifa la Iraq.
Aidha amesema kuwa Fikra za viongozi wa dini wakishirikiana na kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kamwe hawatatoa ruhusa kwa Marekani kutengeza kiota chao nchini Iraq na mashariki ya kati kwa ujumla.
Alhaidariy amesema kuwa Iraq na wananchi wake wanajifaharisha kwa kupata ushindi dhidi ya vikundi vya kigaidi nchini humo, katika hali ambayo miaka arubaini ya mapinduzi ya kiislamu ya Iran yametuthibitishia kwamba kuwa na msimamo na kujiamini na kutegemea uchumi wa ndani alkadhalika kutowaamini maadui zetu ni katika mambo yanayoweza kuifikahsa jamii katika kilele cha ukamilifu.
mwisho/290
10 Februari 2019 - 05:45
Msimbo wa Habari: 928425
Hayo yamesemwa na msaidizi wa masuala ya tamaduni katika taasisi ya Hashdu Shaabiy nchini Iraq na kusisitiza kuwa wamarekani wanapaswa wafahamu kuwa hawana nafasi yeyote nchini humo