17 Februari 2019 - 14:03
Mmoja kati ya vinongozi wa Daesh akamatwa Lebanon

Majeshi ya ulinzi na usalama ya Lebanon yametagaza kumkamata mmoja kati ya viongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo akiwa pamoja na magaidi wengine kadhaa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya ulinzi na uslama nchini Lebanon yamemtia mbaroni kiongozi mmoja wa kikundi cha kigaidi cha Daesh akiwa pamoja na magaidi wengine kufuatia msako uliofanywa na majeshi hayo nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti hii niu kwamba mmoja kati ya waliokamatwa ni katika viongozi wa kikundi hicho ambapo waliingia nchini humo kinyume na sheria kupia moja kati ya boda ya taifa hilo.
Aidha wiki iliopita majeshi ya Lebanon yaliamua kufunda mipaka na Boda zote zinazotumika kuingia watu nchini humo kinyume na sheria, ambapo magaidi wengi waliopo nchini Syria walikuwa wakitumea mwanya huo kuingia nchini Lebanon kinyume na sheria.
Ama majeshi ya Lebanon yamesisitiza sababu za kufunga mipaka hiyo kwamba pamoja ya kuzuia kuingia kwa magaidi nchini humo, sababu nyingine pia nikuzuia ufanyaji wa biashara haramu unaofanyika kupitia mipaka hiyo.
mwisho/290