ABNA: Maelfu ya raia wa Sudan wamefanya maandamano makubwa na kufurika mjini Khartoum kushinikiza watawala wa kijeshi kuachia madaraka. Waandamanaji wamepiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi katikati ya mji mkuu, Khartoum tangu April 6, ambapo hapo kabla waliongoza shinikizo la kumtoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir. Licha ya jumuiya ya kimataifa kuwaunga mkono waandamanaji, baraza la kijeshi lenye wajumbe kumi limesalia madarakani ingawa wajumbe watatu walijiuzulu mnamo siku ya Jumatano kutona na shinikizo mitaani. Waandamanaji walipaza sauti wakisema "Uhuru, Uhuru" wakati Imam Matter Younis alipokuwa akihutubia kabla ya sala ya Ijumaa. Viongozi wa makundi ya waandamanji wamefanya mikutano kadhaa na baraza la kijeshi na kufikia makubalino ya kuunda kamati ya pamoja kutafuta mwelekeo wa siku zijazo, lakini hakuna mafanikio hadi sasa.
Mwisho wa habari / 291