(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, katu Wairani hawatasalimu amri mbele ya vitendo vya mabavu na ubeberu wa adui.
Rais Rouhani amesema hayo katika mkutano wake na wanaharakati wa masuala ya utamaduni na sanaa hapa nchini na kubainisha kwamba, Wairani ni watu wa mazungumzo na mantiki, lakini wanayaona madai ya upande wa pili ya eti utaifanya Iran ilazimike kukaa katika meza ya mazungumzo kwamba, hayana msingi wowote.
Rais Rouhani amesisitiza kuwa, Wairani hawako tayari kufanya mazungumzo kama haya hata kama madola yote makubwa duniani yatashirikiana na kuwa kitu kimoja.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, hii leo ukiondoa nchi tatu mpaka nne hivi pamoja na utawala haramu wa Israel hakuna taifa linaloyakubali maneno ya Marekani.
Rais Hassan Rouhani amesisitiza kuwa, ni jambo lisilo na shaka kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itapata ushindi mbele ya adui.
Jumatano iliyopita, Rais Donald Trump wa Marekani alidai kwamba, muda si mrefu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakaa katika meza moja ya mazungumzo na serikali ya Washington.
Hivi karibuni, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alifutilia mbali pia uwezekano wa kufanyika mazungumzo kati Tehran na Washington kutokana na kile alichokitaja kama mienendo na sera za uhasama na uadui za Marekani dhidi ya Iran.
/129
19 Mei 2019 - 08:09
Msimbo wa Habari: 942495
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, katu Wairani hawatasalimu amri mbele ya vitendo vya mabavu na ubeberu wa adui.