(ABNA24.com) Harakati ya wananchi ya Ansarullah ikishirikiana na vikosi vya Yemen vimefanikiwa kudhibiti maeneo muhimu zaidi ya 20 katika mkoa wa kusini mwa Saudia Arabia wa Najran, sambamba na kuwapa kipigo kikali wapiganaji mamluki wa Saudia.
Msemaji wa Ansarullah, Yahya Sarei amesema maeneo 20 muhimu ya kijeshi ya Saudia kwa sasa yanadhibitiwa na wanamapambano wa Ansarullah baada ya kutekeleza operesheni kabembe, na kwamba mamia ya mamluki wameuawa na kujeruhiwa katika operesheni hiyo ya kushtukiza.
Amefafanua kuwa,"Operesheni hiyo ya siku 3 mbali na kutoa pigo kwa Saudia, lakini pia imewapa ushindi mkubwa wapiganaji wa kujitolea wa Yemen. Kwa sasa tunadhibiti zaidi ya maeneo 20 ya kistratajia ndani ya ardhi ya Saudia."
Amesema vikosi hivyo vya wananchi vimefanikiwa kuangamiza au kujeruhi mamluiki zaidi ya 200 katika operesheni hiyo iliyofanyika katika mkoa wa Najran, mpakani mwa nchi mbili hizo.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, Jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa nchi hiyo vilijibu mashambulizi ya mfululizo ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya wananchi Waislamu wa Yemen, kwa kushambulia uwanja wa ndege wa Najran kwa kutumia ndege isiyo na rubani.
Wayemen wamekuwa wakisisitiza kuwa, mashambulizi ndani ya ardhi ya Saudi Arabia ni haki yao katika kujibu jinai zinazofanywa na wavamizi hao dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Yemen.
Ikumbukwe kuwa Saudia ilianzisha hujuma yake dhidi ya Yemen mnamo Machi mwaka 2015 kwa lengo la kuirejesha madarakani serikali kibaraka ya Abdu Rabuh Mansour Hadi aliyejiuzulu urais na kukimbilia mji mkuu wa Saudia, Riyadh, ambapo watu zaidi ya 14,000 wameuawa na mamilioni ya wengine kujeruhiwa.
/129
8 Juni 2019 - 05:16
Msimbo wa Habari: 948022
Harakati ya wananchi ya Ansarullah ikishirikiana na vikosi vya Yemen vimefanikiwa kudhibiti maeneo muhimu zaidi ya 20 katika mkoa wa kusini mwa Saudia Arabia wa Najran, sambamba na kuwapa kipigo kikali wapiganaji mamluki wa Saudia.