(ABNA24.com) Kamanda wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali wanaojulikana kwa jina la MINUSMA amelaani mauaji ya raia yaliyofanywa katika kijiji kimoja cha katikati mwa nchi hiyo na kutoa mwito wa kuchukuliwa hatua kali za kukabiliana na vitendo kama hivyo.
Televisheni ya France 24 imetangaza habari hiyo na kumnukuu Mehmet Saleh Anadif, kamanda wa kikosi cha MINUSMA akisema kuwa wakati umefika wa kuchukuliwa hatua kali za kupambana na vitendo vya mauaji na machafuko nchini Mali.
Hata Rais Ibrahim Boubacar Keïta wa Mali naye amehimiza kuchukuliwa hatua kali kimataifa kwa ajili ya kukomesha vitendo vya mauaji na machafuko nchni mwake.
Kijiji kimoja cha watu wa kabila la Dogon huko katikati ya Mali, Jumamosi usiku kilivamiwa na watu wenye silaha ambao waliua watu wapatao mia moja wa kabila hilo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wiki chache zilizopita pia, kulifanyika mashambulizi dhidi ya kabila jingine la Pol Futa nchini Mali na kuuliwa watu 160 wa kabila hilo.
Maeneo ya kaskazini na katikati mwa Mali yamekumbwa na machafuko mengi katika miezi ya hivi karibuni.
Mapigano katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika yalishadidi mwaka 2012 baada ya wanajeshi kufanya mapinduzi yaliyoiondoa madarakani serikali ya kiraia na kutoa mwanya wa kutokea uasi wa kila namna hasa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Magenge ya kigaidi nayo yalitumia fursa hiyo kujipenyeza nchini Mali na tangu wakati huo hadi hivi sasa yamekuwa yakifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia wa kawaida.
/129
12 Juni 2019 - 09:11
Msimbo wa Habari: 950160
Kamanda wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali wanaojulikana kwa jina la MINUSMA amelaani mauaji ya raia yaliyofanywa katika kijiji kimoja cha katikati mwa nchi hiyo na kutoa mwito wa kuchukuliwa hatua kali za kukabiliana na vitendo kama hivyo.