22 Juni 2019 - 06:18
Kombora la Cruz la jeshi la Yemen lakilenga kituo cha umeme kusini mwa Saudia

Jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen leo asubuhi yamevurumisha kombora la cruz na kukilenga kituo cha nguvu za umeme cha al Shuqaiq mkoani Jizan kusini mwa Saudi Arabia.

(ABNA24.com)  Jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen leo asubuhi yamevurumisha kombora la cruz na kukilenga kituo cha nguvu za umeme cha al Shuqaiq mkoani Jizan kusini mwa Saudi Arabia.

Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema kuwa kombora hilo la cruz limepiga kwa usahihi shabaha iliyokusudiwa na kwamba shambulizi hilo limefanywa kujibu jinai za muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia. Brigedia Jenerali Yahya Saree amesisitiza kuwa Wayemeni wameaandaa mipango maalumu ya kuzishambulia taasisi muhimu huko Saudia. Jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen jana Jumatano pia yalishambulai eneo walipokuwa wamekusanyika mamluki wa Saudia karibu na kivuko kimoja mkoani Asir kusini mwa Saudia kwa kutumia kombora lililoundwa na wataalamu wa Yemen aina ya Zilzala-2.

Makumi ya mamluki wa Saudi Arabia waliuliwa na kujeruhiwa. Viongozi wa Yemen wamesisitiza kuwa ngome na vile vile taasisi za kiuchumi za nchi vamizi huko Yemen zitakabiliwa na mashambulizi mtawalia ya makombora madhali zingali zinaizingira nchi hiyo na kuendeleza mashambulizi yao nchini humo. Utawala wa Saudia na waitifaki wake wameshindwa kufikia malengo yao ya kuurejesha utawala kibaraka wanaoutaka wao huko Yemen kutokana na muqawama na kusimama imara wananchi wa Yemen dhidi ya wavamizi.



/129