22 Julai 2019 - 05:46
 Muhammad Ali al-Houthi: Marekani chanzo kikuu cha matatizo ya wananchi wa Yemen

Mousavi: Pendekezo la mazungumzo la Marekani ni hila ya kukamilisha njama zake dhidi ya Iran

(ABNA24.com) Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, pendekezo la Marekani la kutaka kufanya mazungumzo na Iran ni hila tu ya kujaribu kukamilisha njama za Washington dhidi ya Tehran yaani kuliwekea taifa la Iran mashinikizo makubwa kupindukia.

Sayyid Abbas Mousavi amesema hayo katika mahojiano na gazeti la al Akhbar la Lebanon. Mahojiano hayo yamechapishwa leo Jumamosi. Ameongeza kuwa, kitendo cha Marekani cha kujitoa bila sababu katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kufanya njama za kuzishawishi nchi za Ulaya zijitoe kwenye makubaliano hayo ya kimataifa, kuiwekea vikwazo Iran kwa awamu kadhaa, kuvunja waziwazi azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na vitendo vingine mbalimbali vya kiuadui vya Marekani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, yote hayo yanaifanya Iran ikatae katakata kufanya mazungumzo na Marekani.

Vile vile amesisitiza kuwa, Tehran itaendelea na mchakato wake wa kupunguza utekelezaji wa ahadi zake ndani ya JCPOA na kuongeza kuwa: Muda wote Iran imekuwa ikizitahadharisha nchi za Ulaya kuhusu madhara makubwa ya kusambaratika mapatano hayo ya kimataifa, kujitoa Marekani kwenye makubaliano hayo na kutoheshimu nchi za Ulaya ahadi zao ndani ya JCPOA.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, kuendelea kuwepo wanajeshi wa kigeni katika eneo la Asia Magharibi ndiko kunakoongeza uwezekano wa kutokea vita kwenye eneo hili.

Vile vile amesema, Iran kamwe haitokuwa ya kwanza kuanzisha vita lakini kama itachokozwa basi itasimama imara kujilinda kwa nuguvu zake zote na kwamba hakuna hatua yoyote ya Marekani itakayoachwa vivi hivi bila ya kujibiwa.



/129