(ABNA24.com) Rais Erdoğan ameyasema hayo jana katika kikao na wajumbe wa chama cha Uadilifu na Ustawi mjini Ankara wakati akielezea kitendo cha serikali ya Marekani cha kukatakaa kuikabidhi Uturuki ndege za kivita aina ya F35 na kuongeza kwamba anataraji kuwa Washington itaamiliana na suala hilo kwa akili na busara. Amesema Uturuki inafungamana na mkataba wa malipo ya Dola bilioni moja na milioni 400 ilizozitoa kwa ajili ya mradi huo na kwamba iwapo Marekani haitoikabidhi serikali ya Ankara ndege hizo za kivita, basi italazimika kurejea machaguo mengine kwa lengo la kujidhaminia silaha.
Makabidhiano ya shehena ya mfumo wa ngao ya makombora wa S 400 wa Russia yalianza tarehe 12 mwezi huu. Mkataba wa mauziano ya ngao hiyo ya makombora ulitiwa saini Disemba 2017 kati ya Uturuki na Russia. Hapo awali serikali ya Marekani ilitangaza kwamba iwapo Uturuki haitobadili azma yake ya kununua ngao hiyo ya makombora kutoka Russia, basi Washington itafuta mkataba wa kuikabidhi nchi hiyo ndege za kivita aina ya F35.
/129