28 Julai 2019 - 07:26
Rais Tayyip Erdoğan: Uturuki inajitahidi kuleta umoja katika ulimwengu wa Kiislamu

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema kuwa serikali ya Ankara inajitahidi kuleta umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.

(ABNA24.com) Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema kuwa serikali ya Ankara inajitahidi kuleta umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.

Rais Erdoğan ameyasema hayo katika kikao na waandishi wa habari akiwa na Mahathir Bin Mohamad, Waziri Mkuu wa Malaysia mjini Ankara na kuongeza kwamba umoja na mshikamano wa ulimwengu wa Kiislamu ni suala muhimu kwa serikali ya Ankara. Kadhalika rais huyo wa Uturuki amesisitiza kwamba, njia pekee ya kukabiliana na njama za maadui za kuleta mifarakano, ni kuwa makini, kuwa na uelewa na kuwepo umoja wa ulimwengu wa Kiislamu.

Wakati huo huo, Mawaziri wa Ulinzi wa Uturuki na Malaysia wamekutana na kujadiliana njia za kustawisha ushirikiano wao wa kijeshi. Katika mazungumzo hayo, Mohamad Sabu wa Malaysia na Hulusi Akar wa Uturuki, wamezungumzia uhusiano wa pande mbili kuhusu kustawisha ushirikiano wa nchi mbili katika sekta ya ulinzi na kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na usalama baina yao. Waziri wa Ulinzi wa Malaysia aliwasili Uturuki akiandamana na Mahathir Bin Mohamad, Waziri Mkuu wa nchi hiyo.



/129