(ABNA24.com) Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria muqawama na kusimama kidete wananchi wa Syria, Lebanon, Iraq, Bahrain na Yemen mbele ya Waistikabari na kusisitiza kuwa, muqawama wa wananchi wa eneo la Mashariki ya Kati chimbuko lake ni somo la Ashura na harakati ya Imam Hussein AS.
Hujatul-Islam Wal-Muslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi Fard amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran ambapo amebainisha kwamba, katika kipindi cha miaka Arobaini iliyopita, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamepata ushindi wa kukumbukwa kupitia shule na somo la Ashura.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameongeza kuwa, shule ya Ashura hii leo imeibadilisha jamii ya mwanadamu na kuifanya kuwa jamii yenye utamaduni wa mapinduzi, kusimama kidete na kutosalimu amri mbele ya dhulma na ukandamizaji wa mabeberu.
Hujatul-Islam Wal-Muslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi Fard amesema pia kuwa, Waislamu wanapaswa kumtambua adui na kueleza kwamba, Marekani na Waistikbari wa dunia wana wasiwasi mno na ushindi wa kambi ya muqawama na mapambano.
Kadhalika khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran ameashiria vikawzo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza wazi kwamba, kupata somo na funzo kupitia tukio la Ashura na harakati ya Imam Hussein (as) kutapelekea kupata ushindi katika vita vya kiuchumi vya kila upande vya madola ya Magharibi.
/129
14 Septemba 2019 - 06:37
Msimbo wa Habari: 975242
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria muqawama na kusimama kidete wananchi wa Syria, Lebanon, Iraq, Bahrain na Yemen mbele ya Waistikabari na kusisitiza kuwa, muqawama wa wananchi wa eneo la Mashariki ya Kati chimbuko lake ni somo la Ashura na harakati ya Imam Hussein AS.