5 Oktoba 2019 - 09:32
Ayatullah Kashani: Matembezi ya mamilioni katika Arubaini ya Imam Hussein AS yatafana zaidi

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameashiria machafuko ya hivi karibuni nchini Iraq na kuhusika maadui katika kuibua ghasia hizo na kusema: "Maadui wanajaribu kuvuruga matembezi ya mamilioni ya watu katika Arubaini ya ya Imam Hussein AS lakini matembezi hayo yatafana na kuwa makubwa zaidi mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliyopita.

(ABNA24.com) Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameashiria machafuko ya hivi karibuni nchini Iraq na kuhusika maadui katika kuibua ghasia hizo na kusema: "Maadui wanajaribu kuvuruga matembezi ya mamilioni ya watu katika Arubaini ya ya Imam Hussein AS lakini matembezi hayo yatafana na kuwa makubwa zaidi mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Katika siku za hivi karibuni, maeneo kadhaa ya Iraq, ukiwemo mji mkuu wa Iraq, yameshuhudia maandamano makubwa ya watu wanaolalamikia hali mbaya ya kimaisha, ukosefu wa ajira na ufisadi katika idara za umma. Uchunguzi umebaini kuwa maandamano hayo yalichochewa na maadui wa taifa la Iraq.

Ayatullah Mohammad Imami Kashani, katika hotuba zake za Swala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran amesema, bendera ya Imam Hussein AS, Imamu wa Tatu wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia duniani, ni bendera ya kupambana na dhulma. Ameongeza kuwa: "Marekani na utawala wa Kizayuni zinatekeleza njama za kuficha ukweli na uhakika."

Ayatullah Imami Kashani aidha ameashiria ushundi wa watu waliodhulumiwa wa Yemen dhidi ya wavamizi na kusema: "Ushindi wa watu wa Yemen ni jambo ambalo limeufedhehesha utawala wa Saudia na waitifaki wake."

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ameashiria pia mashinikizo ya Marekani dhidi ya Iran na kusema, kwa kusimama kidete watu wa Iran, mashinikizo ya juu zaidi ya adui yamebadilika na kuwa fedheha ya juu zaidi kwa adui."


/129