(ABNA24.com) Gazeti hilo limeandika habari hiyo wakati likichambua uhusiano baina ya Jordan na Israel na kusema kuwa, licha ya kwamba zaidi ya miongo miwili imepita tangu kutiwe saini makubaliano ya amani baina ya pande mbili, lakini vitendo vya utawala wa Kizayuni vimezidisha hasira za wananchi wa Jordan ambao wanaiona Israel ni adui yao mkubwa asiyevumilika.
Kwa mujibu wa gazeti hilo la Kizayuni, serikali ya Jordan hivi sasa imejikuta iko njia panda. Moja ya njia hizo ni kambi inayoongozwa na rais wa Marekani, Donald Trump ya watu wanaojivutia kila kitu upande wao na njia ya pili ni msimamo wa wananchi ndani ya Jordan ambao kila kukicha wanazidi kuuchukia utawala wa Kizayuni na wanaitaka nchi yao ikate kikamilifu uhusiano wake wa kibiashara na kidiplomasia na Israel.
Wananchi wa Jordan wanaziona jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia huko Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Vile vile wananchi hao wanaamini kuwa, Trump na Israel wanafanya njama za kuvuruga na kufuta kabisa utambulisho wa kihistoria wa Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa.
Sababu nyingine ni kwamba malengo yote yaliyotangazwa katika makubaliano ya amani baina ya Jordan na Israel hakuna hata moja lililofanikishwa licha ya kupita miaka 25 sasa tangu yaliyopitwa saini.
.........
340