(ABNA24.com) Akizungumza Alhamisi katika kikao cha Bodi ya Magavana wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Kazem Gharibabadi aliwasilisha ripoti kuhusu misimamo ya hivi karibuni ya Tehran kuhusu JCPOA na kuyataja kuwa yasiyo na msingi madai ya uwezekano wa kukengeuka mkondo wa shughuli za nyuklia za Iran.
Gharibabadi ambaye pia ni balozi wa Iran katika IAEA ametupilia mbali madai ya Marekani ya kufanya mazungumzo na Iran. Amesema Marekani imetoa madai hayo ili kukwepa majukumu yake ya kimataifa.
Aidha amesisitiza kuwa, kama ambavyo Iran imetangaza mara kadhaa, silaha za atomiki hazina nafasi katika sera zake za usalama na kujihami.
Gharibabadi aidha amesema Marekani inatoa madai dhidi ya shughuli za nyuklia za Iran katika hali ambayo Tehran imeonyesha nia njema kupitia utekelezwaji wa ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na dunia imeweza kushuhudia namna ambavyo IAEA imewasilisha ripoti zinazoonyesha kuwa Iran imefungamana na ahadi zake katika JCPOA.
.........
340