(ABNA24.com) Nchi hiyo ya kusini magharibi mwa Afrika ilifanya uchaguzi wake wa sita wa rais na bunge Jumatano huku ikiwa inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi.
Chama cha SWAPO, ambacho ni chama cha rais Geingob, kimekuwa madarakani tokea Namibia ipate uhuru wake kutoka Afrika Kusini mwaka 1990 na kingali kinaheshimiwa kutokana na nafasi yake kubwa katika ukombozi wa nchi hiyo.
Pamoja na hayo, Rais Geingob ambaye alichaguliwa kwa asilimia 87 ya kura mwaka 2014, anatazamiwa kupoteza idadi kubwa ya kura baada ya mwanachama maarufu wa SWAPO, Panduleni Itula kuamua kuwania urais kama mgombea huru. Itula ameweza kupata umashuhuri miongoni mwa vijana wa Namibia, ambao nusu yao hawana ajira.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali, Rais Geingob, atabakia kuwa rais lakini amepoteza uungaji mkono katika miji mikubwa.
Kuna uwezekano kuwa ushindi wa SWAPO utapingwa katika mahakama baada ya wapinzani kudai kuwa utumizi wa mashine za kielektroniki katika upigaji kura umepelekea kuwepo uchakachuaji katika uchaguzi huo.
.........
340