(ABNA24.com) Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Mohammad-Hassan Aboutorabi Fard ameyasema hayo katika hotuba ya sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo na kusisitiza kwamba, kusimama imara mbele ya Marekani maana yake ni kupiga hatua katika njia ya uzalishaji elimu, kubuni teknolojia na kuijenga Iran yenye nguvu na kiwango cha juu kabisa cha pato la kila mtu. Ameongeza kwa kusema kuwa njia hiyo itaweza kufikiwa tu kwa kupatikana teknolojia ya kisasa na kwa kuweza kuuza elimu.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, hatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran sambamba na kuashiria utekelezwaji wa mpango wa marekebisho ya bei ya mafuta amesema kuwa, haikupasa kuruhusu suala hilo muhimu na nyeti, ambalo lingeweza kuwaunganisha pamoja shakhsia wenye vipawa wa kisiasa na kielimu na kuungwa mkono na wananchi wa Iran na hivyo kuwa ramani ya njia kwa ajili ya umoja na nguvu za kitaifa, litumiwe vibaya na maajinabi na idara zao za intelejensia na ujasusi.
Aidha Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Mohammad-Hassan Aboutorabi Fard amesisitiza kwamba kuyapa umuhimu na kufuatilia matatizo ya familia zilizoathirika na matukio ya hivi karibuni, ni kipaumbele cha viongozi wote wa serikali.
.........
340