(ABNA24.com) Sambamba na kuendelea mashauriano ya Hassan Diab ambaye sasa ana jukumu la kuunda serikali mpya huko Lebanon; Gebran Basil ameeleza kuwa pande na mirengo yote ya kisiasa ya nchi hiyo inapasa kuunga mkono mchakato huo. Amesema lengo lao zaidi ni kuunga mkono kuteuliwa mawaziri wasio wanasiasa, wasiokabiliwa na ufisadi na wenye kukidhi viwango.
Gebran Basil amesisitiza kuwa marekebisho na mabadiliko yanapasa kutekelezwa ndani ya serikali; na kunapasa kuwepo uchumi wenye tija ambao utaweza kukabiliana ipasavyo na suala la ufisadi.
Hassan Diab hatimaye amepewa jukumu la kuunda serikali huko Lebanon kwa kuungwa mkono na kura 69 kati ya jumla ya kura 128 baada ya mashauriano kati ya Rais wa nchi hiyo Michel Aoun na bunge.
Diab amesisitiza kuwa hataruhusu hali ya mambo ya Lebanon irejee kama ile ya kabla ya Oktoba 17. Amesema ujenzi wa mustakbali wa nchi unawezekana tu kwa kushughulikia matakwa ya wananchi.
..........
340