-
Al_Itrah Foundation, Dar-es-salaam - Tanzania yampa zawadi ya Tafsiri ya Kiswahili ya Qur'an Tukufu Mwenyekiti wa JMAT - TAIFA Sh.Dr Alhad Mussa Salum
"Kitabu Hicho Hakina Shaka ndani yake, ni Muongozo kwa Wacha Mungu".
-
Habari Pichani | Qaswida ya kumsifu Mtume Muhammad | "Haya Tumpendeni Nabiyya" - Lamada Hotel, Ilala -Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Waumini wengi wa Kiislamu wamehudhuria kwa hamasa kubwa katika Ukumbi wa Lamada Hotel - Ilala, Dar-es-salaam - Tanzania, ili kusikiliza Qaswida ya mbalimbali za Kumsifu Mtume Muhammad (saww) na kuonyesha Mapenzi Yao makubwa juu yake. Qaswida hizo zilisomwa Mubashara kwa Sauti nzuri na zenye Mahadhi mbalimbali ya Kiushairi. Qaswida zote ziliwakonga nyoyo Waislamu, ni pamoja na Qaswida ya: "Haya tumpendeni Nabiyyah"... Mahaba ya Amini hayazuiliki nyoyoni. Ametuathiri Sana Nabiyyah nyoyoni. Sote twataraji kwako kupata Shifaa yako". Qaswida hii imewakonga nyoyo Waislamu wengi Tanzania wenye Mapenzi makubwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Qaswida hii zingine nyingi zilisomwa na kundi la Qaswida la Ahlu - Zaman 2025.
-
Ziara ya Kiilmu na Maarifa katika Hawzat Imam Ali (a.s) Pangani, Tanga - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sheikh Kadhim Abbas, Mudir wa Hawza za Bilal Muslim Tanga, Tanzania, leo hii Alhamisi Machi 10, 2025 amefanya akiwa ziarani katika Hawza ya Imam Ali (a.s) Pangani. Ziara hii ina lengo kuboresha Sekta ya Elimu na Maarifa ya Kiislamu katika Hawza zote za Bilal Muslim Tanga - Tanzania. Ametoa nasaha muhimu kwa Wanafunzi wa Hawzah akisema: "Wanafunzi wa Kidini wanapaswa kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo yao ili kuhakikisha wanayafikia malengo matukufu ya kuchuma Elimu na Maarifa ya Dini Tukufu ya Kiislamu".
-
Russia: Dunia imechoshwa na vitisho visivyokwisha vya Marekani dhidi ya Iran
Russia imelaani vikali vitisho vya mara kwa mara vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema dunia imechoshwa na hali hiyo.
-
Sera za ushuru za Trump na ukuruba wa China na Ulaya
Sera za ushuru za Rais Donald Trump wa Marekani zimegeuka kuwa vita vya kibiashara kati ya Marekani na waitifaki, washirika na wapinzani wake wa kibiashara.
-
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza: Trump anaiburuta dunia katika ukingo wa mdodoro wa uchumi
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ametahadharisha kuwa sera za kibiashara za Rais Donald Trump wa Marekani zinauelekeza uchumi wa dunia katika mdodoro hatari wa kiuchumi; na ni kupitia tu kuratibiwa hatua za kimataifa ndipo tunaweza kuzuia kukaririwa mgogoro wa uchumi kama ule ulioiathiri dunia mwaka 2008.
-
Viongozi wa Amerika ya Latini watoa wito kupinga ushuru wa Trump
Viongozi wa nchi za Amerika ya Latini wametaka kuweko umoja na mshikamano wa kukabiliana na ushuru wa Rais Donald Trump wa Marekani na kuyumba uchumi kunakosababishwa na hatua hizo za Trump.
-
Wapalestina wengine 40 wauawa shahidi Gaza na mabomu ya Wazayuni
Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kumwaga damu za Wapalestina; ambapo umewauwa Wapalestina karibu 40 wakiwemo watoto katika mashambulizi ya anga ya karibuni katika maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
-
Microsoft yalaaniwa kwa kumfuta kazi mhandisi aliyepinga mauaji ya kimbari Gaza
Shirika moja la kimataifa limelaani hatua ya kampuni ya Microsoft ya Marekani kumfuta kazi mhandisi wa programu mwenye asili ya Morocco, Ibtihal Aboussad, ambaye aliandamana hadharani kupinga uungwaji mkono wa kampuni hiyo kwa utawala katili wa Israel wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Microsoft.
-
Ansarullah yaitahadharisha Marekani kuhusu vita vya nchi kavu dhidi ya Yemen
Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Ansarullh ya Yemen amelaani mashamulizi ya anga ya Marekani nchini humo na kutahadharisha kuhusu hatua yoyote ya kijeshi ya nchi kavu ya Washington dhidi ya Yemen.
-
Maariv : Hamas bado inadhibiti Ukanda wa Gaza
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimekiri kuwa, zaidi ya mwaka mmoja na nusu tangu kuanza vita na mshambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukanda wa Gaza, harakati ya Hamas bado inadhibiti eneo hilo na utawala wa Kizayuni umeshindwa kufikia malengo yake.
-
Kuidhinishwa makubaliano ya pande zote baina ya Iran na Russia katika Duma kuna umuhimu gani?
Bunge la Duma la Russia Jumanne (Aprili 8) liliidhinisha Mkataba wa Ushirikiano Kamili wa Kimkakati kati ya Russia na Iran.
-
Iran: Nyuklia na kuondolewa vikwazo ndizo maudhui pekee za mazungumzo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: Suala la nyuklia kwa maana ya kuhakikisha mradi wa nyuklia wa Iran ni wa amani kikamilifu na kuondolewa vikwazo, ndiyo masuala pekee yanyojadiliwa kwenye mazungumzo.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Misri wasisitiza ulazima wa kukomesha jinai Israel Gaza
Iran imetoa wito kwa nchi za eneo kushirikiana kuchukua hatua za haraka kukomesha uhalifu wa utawala wa Israel na kufufua makubaliano ya usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza.
-
Araqchi: Uhusiano wa Iran na Algeria uko imara, ni wa kihistoria
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Algeria ni nchi kubwa na yenye taathira katika Ulimwengu wa Kiislamu na kwamba uhusiano kati ya nchi hiyo na Iran ni mkubwa, imara na wa siku nyingi.
-
Uwezo wa kuthamini na kuheshimu vipengele viwili vya Imani na Utamaduni / Jinsi jamii ya Wairani nchini Tanzania inavyo balansi Imani na Utamaduni
Nyakati kama hizo hutoa somo muhimu katika kuishi pamoja Kitamaduni na kwa utangamano wa Kidini, na hili sio kwa Wairan tu, bali ni kwa Jamii ya Kimataifa.
-
Samahat Sheikh Kadhim Abbas, Mudir wa Hawza za Bilal Muslim Tanga - Tanzania, amefanya ziara muhimu katika Hawza ya Imam Ali (a.s)
Sheikh Kadhim ametoa akitoa nasaha kwa nasaha kwa Wanafunzi amesema: "Wanafunzi wa Kidini wanapaswa kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo yao ili kuhakikisha wanayafikia malengo matukufu ya kuchuma Elimu na Maarifa ya Dini Tukufu ya Kiislamu".
-
Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria yalaani Serikali kwa mauaji ya Waandamanaji 26 wanaounga mkono Palestina, na kuwaweka kizuizini 274
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, matukio kadhaa ya amani ya kidini yaliyoandaliwa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria chini ya uongozi wa Sheikh Zakzaky, likiwemo Kongamano la Mwaka la Mauaji ya Zaria ya mwaka 2015 na programu ya Nisfu / Nusu Sha’ban kwa ajili ya kuadhimisha Maulid ya Imam Mahdi (a.t.f.s), yaliripotiwa kuvurugwa na vikosi vya usalama.
-
Nukta 7 na Muhimu za Tabia Njema, Zilizosheheni Hekima na Busara
"Mwenyezi Mungu ameumba Viumbe Tofauti tofauti, na kila kimoja amekipa sifa zake , Ni Tatizo sana unapo taka Sifa za Kuku awenazo Bata".
-
Habari Pichani | Madrasat Imam Baqir (a.s) Tanzania | Ujenzi wa Madrasat hii unaendelea eneo la Utete - Tanzania.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Ujenzi wa Madrasat Imam Baqir (a.s) unaendelea (9/4/2025). Katika picha hizi, ujenzi huo umefikia katika hatua ya kupaua. Hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamilika kwa hatua ya kuinua kuta za jengo husika. Madrasat hii inayojengwa inaitwa kwa Jina la Imam Baqir (a.s), ambapo inajengwa chini ya Usimamizi na Uongozi wa Samahat Sayyid Arif Naqvi, Mkuu wa Taasisi Hojjat-ul- Asr Society Of Tanzania.