Martin Griffiths ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kuwa mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni juzi usiku yameuwa makumi ya watu aghalabu yao wakiwa ni wanawake na watoto ambao wameungua wakiwa hai.
Mratibu mkuu wa misaada na masuala ya dharura wa UN ameashiria changamoto zinazowakabili katika kusambaza misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa: "Bado tumeshindwa kufikisha kiwango kinachohitajika cha bidhaa za mahitaji huko Kerem Shalom kufuata kuendelea mashambulizi na vita huko Gaza."
Griffiths ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za dharura ili kuwalinda raia na kuhakikisha usalama wao. Watu wasiopungua 45 wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameuawa shahidi na wengine karibu 250 kujeruhiwa juzi Jumapili katika mashambulizi ya anga ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya vituo na kambi za wakimbizi wa Kipalestina katika mji wa Rafah.Utawala haramu wa Israel umetekeleza mashambulizi hayo tajwa katika mji wa Rafah licha ya uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ulioamuru Israel kusimamisha mashambulizi yake katika mji wa Rafah mara moja.
342/