Ofisi ya uwakilishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa imeeleza katika taarifa iliyotoa Ijumaa kwamba Tehran inauchukulia kuwa si ubinadamu usaidizi wowote wa kijeshi unaotolewa kwa pande hasimu katika vita vya Ukraine, usaidizi ambao unaongeza maafa ya roho za watu na uharibifu wa miundombinu nchini Ukraine. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kwa sababu hiyo, sio tu Jamhuri ya Kiislamu haifanyi jambo kama hilo, lakini pia inazotolea mwito nchi zingine kuacha kuzipatia silaha pande zinazohusika katika vita hivyo. Ofisi ya uwakilishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa imesisitiza kwa kusema: msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu mzozo wa Ukraine haujabadilika.Sisitizo hilo limetolewa baada ya wajumbe wa Marekani, Uingereza na Ufaransa kutoa shutuma zilizoratibiwa kwa pamoja dhidi ya Tehran kuhusu mzozo unaoendelea kati ya Russia na Ukraine, wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika Agosti 30.
Tehran imeshakanusha mara kadhaa madai ya Magharibi kwamba inajihusisha na vita kati ya Russia na Ukraine.
Aidha, Iran imekuwa ikitoa mwito wa kusitishwa mapigano na kusisitiza kuwa kuendelea vita nchini Ukraine kunachangiwa zaidi na upelekaji silaha nchini humo unaofanywa na nchi za Magharibi.../
342/