Kwa mujibu wa IRNA, Rais Pezeshkian amewasili katika eneo la Kurdistan leo Alkhamisi katika siku ya pili ya safari yake nchini Iraq, na kukaribishwa na rais wa eneo hilo, Nichervan Barzani. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye jana (Jumatano) alisafiri kuelekea Iraq kwa ziara ya siku tatu, amesema katika mahojiano na kanali ya habari ya Rudaw kwamba uhusiano kati ya Iran na eneo la Kurdistan hivi sasa ni mzuri na juhudi zinapasa kufanywa ili kuimarisha zaidi uhusiano huo.Jana Jumatano, Rais Pezeshkian alielekea nchini Iraq huku akiongozana na ujumbe wa ngazi za juu wa maafisa wa kisiasa na kiuchumi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kulakiwa na kukaribishwa rasmi na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mohammad Shia al-Sudani alipowasili katika uwanja wa ndege wa Baghdad.
342/