Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kauli iliyochapishwa hivi karibuni imeibua mjadala kuhusu uhusiano wa Waislamu na Mayahudi pamoja na Manaswara, ikiuliza: “Mmejipatiaje ridhaa yao mpaka wakawa na huruma na kuwaunga mkono?”
Kauli hiyo imenukuu Surat Al-Baqarah, Aya ya 120, inayosema kwamba Mayahudi na Manaswara hawataridhika mpaka mtu afuate mila yao, huku ikisisitiza kuwa uongofu wa Allah ndio uongofu wa kweli.
Kwa kutegemea aya hiyo, mwandishi wa kauli hiyo anabainisha kuwa baadhi ya watu wamepata ridhaa ya Mayahudi na Manaswara kwa kuingia chini ya ushawishi wao, na kwamba kwa kufanya hivyo wamepoteza wilaya ya Allah, pamoja na kudai kuwa wamekosa msaada, ushindi, nguvu na heshima.
Kauli hiyo inahitimisha kwa kusisitiza umuhimu wa kutegemea uongofu na msaada wa Allah badala ya kutafuta ridhaa ya nje kwa gharama ya misingi ya imani.
Maoni yako