Shirika hilo limesema mashambulizi ya Hizbullah nchini Lebanon yameongezeka na kushika kasi hususan mwezi huu ambapo yamefikia miji ambayo ilikuwa haijagurwa bado na walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).Jeshi la utawala bandia wa Israeli, ambalo limekuwa likipokea vipigo vikali kutoka kwa Hizbullah ya Lebanon kila siku tangu tarehe 8 mwezi Oktoba mwaka jana hadi sasa, limekuwa likiwalenga kiholela raia wa kawaida kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu katika hatua ya kujaribu kufidia kushindwa kwake kusiko na kifani katika medani ya vita.
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah haijaacha kulipiza kisasi kwa mashambulizi yanayotekelezwa na utawala vamizi wa Kizayuni dhidi ya raia wa Lebanon kwa kutoa mapigo makali ya kijeshi dhidi yake. Katika kukabiliana na jinai hizo imezidisha mashambulizi yake dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na pia maeneo ya jeshi la Kizayuni katika eneo hilo.
Tangu kuanza kwa operesheni za Hizbullah katika eneo la kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala bandia wa Israeli, idadi kubwa ya walowezi wa Kizayuni katika eneo hilo wamelazimika kuyahama makazi yao na kukimbilia mafichoni na kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Kizayuni, wengi wa wakazi wa Kizayuni waliosalia katika eneo hilo wanasumbuliwa na matatizo ya kiakili na kisaikolojia.
342/