29 Januari 2020 - 10:03
Hizbollah Iraq yashakia ushiriki wa Saudia na Imarati katika shambulio la ubalozi wa Marekani

Kufuatia shambulio dhidi ya Ubalozi wa Marekani nchini Iraq, msemaji mkuu wa kikundi cha Hizbollah nchini humo amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba nchi za Saudia na Imarati zikawa na mchango mkubwa katika hilo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:

Kufuatia shambulio dhidi ya Ubalozi wa Marekani nchini Iraq, msemaji mkuu wa kikundi cha Hizbollah nchini humo amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba nchi za Saudia na Imarati zikawa na mchango mkubwa katika hilo.

“Sawa shambulizi dhidi ya Ubalozi wa Marekani ni uharibifu wa wazi kabisa ambao ni zao la ugomvi wa Marekani na Iraq, lakini jambo hili na uharibifu huu unaweza kuwa ni mkono wa Saudia na Imarati..” Jaafar Al Husseiniy msemaji wa kikundi cha Hizollah nchini Iraq alisema.

Katika kuelezea zaidi shaka hiyo Husseiniy amesema kuwa kama mashambulizi hayo yangalikuwa yamepangwa na Iraq yenyewe basi ingekuwa ni kwa sura ya wazi kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa hivyo tangu mwaka 2003 mpaka 2011 na katika sura ambayo Iraq yenyewe inakubali kuhusika na mashambulizi hayo.

Uhusikaji wa Saudia au Imarati katika fujo hizi ni hatua nyingine baada ya kile kinachoaminika kuwa pia walihusika katika kuwajaza chuki wananchi na kisha kuandamana dhidi ya nchi yao huku malengo makuu yakiwa ni kutaka kuwaaminisha Wairaq kuwa kuna umuhimu mkubwa mno wa Majeshi ya Marekani kubakia nchini humo.

Msemaji huyo pia ametoa tanabahi kuwa mashambulizi ya vikosi vyao ni makubwa zaidi ya hayo ambayo yametokea, na jambo hili hata Marekani wenyewe wanajua.

“naweza kusema kwamba laiti tungaliamua kushambulia basi isingekuwa kwa mashambulizi ya juu juu kama haya...” alisema Husseiniy.

Lebo