(ABNA24.com) Mapigano hayo yalitokea jana baada ya msafara wa majeshi ya Uturuki kuingia kwenye mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria.
Kufuatia hatua hiyo ya jeshi la Uturuki ya kuingia kinyume cha sheria mkoani Idlib, jeshi la Syria lilishambulia kwa makombora ya mizinga ngome za jeshi hilo na kuwaua askari sita na kuwajeruhi wengine wapatao 20.
Kwa upande mwingine, askari wasiopungua sita wa Syria wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na jeshi la Uturuki dhidi ya ngome za jeshi hilo.
Tangu siku kadhaa nyuma, jeshi la Syria limeanzisha operesheni ya kuukomboa mji wa Idlib kutoka kwenye makucha ya magaidi.
Sambamba na hatua hiyo, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki alitangaza: 'Kuanzia sasa, na sisi pia tutazilenga ngome za vikosi vya Syria.' Aidha, Erdogan ameitaka Russia, ambayo ni muitifaki wa Syria, isiingilie mashambulio ya Uturuki dhidi ya jeshi la Syria.
Uturuki inadai kuwa wanajeshi wake wako katika eneo la Idlib kwa lengo la kusimamia usitishaji vita.
Hii ni pamoja na kuwa, makundi ya kigaidi yaliyopo katika eneo hilo yamekiuka usitishaji mapigano mara kadhaa na kutenda anuai za jinai katika eneo hilo.
Kufuatia kushambuliwa ngome za jeshi la Uturuki ndani ya ardhi ya Syria, maafisa kadhaa wa serikali ya Ankara akiwemo waziri wa mambo ya nje na msemaji wa rais wamedai kuwa, kushambuliwa ngome za jeshi la Uturuki kumekiuka hati ya makubaliano ya Idlib na kwamba waliohusika na shambulio hilo watakabiliwa na jibu la nchi hiyo.
Ikumbukwe kuwa serikali ya Syria ilishatahadharisha mara kadhaa kuhusu matokeo hasi ya uingiaji kinyume sheria ndani ya ardhi ya nchi hiyo unaofanywa na askari wa Uturuki; na ikatangaza kuwa, uvamizi huo unakiuka mamlaka yake ya kujitawala, hivyo ni lazima Uturuki iondoke katika ardhi ya Syria haraka iwezekanavyo.
...........
340