Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ali Baqeri-Kani amenukuliwa na shirika la habari la Iran Press akisema hayo na kuongeza kuwa: Dunia inapaswa kuubebesha dhima utawala wa Washington kwa mauaji ya kiholela dhidi ya raia.
Baqeri-Kani amegusia kuhusu takwimu rasmi zinazoonyesha kuwa, kwa wastani raia watatu wa Marekani wanauawa kila siku mikononi mwa polisi ya nchi hiyo.
Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria juu ya takwimu rasmi za serikali zinazoonyesha kuwa, asilimia 60 ya watu walioaga dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19 katika jimbo la Chicago nchini Marekani ni Wamarekani wenye asili ya Afrika na kueleza bayana kuwa: sababu kuu ya vifo na mauaji ya raia weusi nchini Marekani ni mfumo wa kibaguzi katika karibu taasisi zote za nchi hiyo.
Afisa huyo wa haki za binadamu wa Iran amebainisha kuwa, hivi sasa imedhihirika wazi kuwa ubeberu wa Marekani haushii tu katika kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyinginezo duniani, lakini pia umeathiri vibaya mfumo mzima wa uongozi ndani ya taifa hilo.
Kwa mujibu wa ripoti, katika kipindi cha miezi minne ya mwanzo wa mwaka huu, zaidi ya raia 200 wamepoteza maisha kutokana na ukandamizaji wa polisi wa Marekani.