Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika kile kinachoonekana kuwa ni kuendelea mvutano mkali ndani ya serikali ya Marekani, maafisa na viongozi mbalimbali wa sasa na wa kabla wameendelea kumkosoa na kumshambulia vikali Ris wa nchi hiyo Donald Trump.
Maafisa na viongozi hao sasa wamejitokeza hadharani na kusema kuwa Trump hafai kabisa kuwa Rais nchi kutokana na kutokuwa na akili wala maadili yanayofaa.
Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani ni kiongozi wa ngazi za juu wa karibuni kabisa ambaye amesema wazi kuwa, akili na maadili yasiyo sahihi aliyonayo Trump yanamuondolea sifa ya kuwa Rais wa nchi.
Aidha John Bolton aliyewahi kuwa mshauri wa usalama wa taifa wa nchi hiyo naye amekariri na kuonyesha msimamo huo huo akibainisha kwamba, Trump hafai kuwa Rais hasa kwa upande wa kiakili na kimaadili.
Hii si mara ya kwa Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani kumkosoa na hata kumshambulia vikali Rais Donald Trump wa nchi hiyo; kwani huko nyuma mara kadhaa amewahi kunukuliwa akimtuhumu Trump kwa kutoa habari na taarifa zisizo sahihi na za uongo.
Katika miezi ya hivi karibuni wimbi la kusolewa Rais Donald Trump wa Marekani limeongezeka mno ndani na nje ya nchi hiyo na kumuweka katika mazingira magumu ya kutetea katika chake katika uchaguzi ujao baadaye Novemba mwaka huu.
342/