Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mashirika mbalimbali yametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, Rais Jair Bolsonaro wa Brazil amelazimika kukubali kuchukuliwa vipimo vya corona baada ya kuonekana na dalili za ugonjwa huo. Ikumbukwe kuwa, rais huyo anafanya ukaidi kama ule wa rais wa Marekani, Donald Trump hasa kuhusu corona. Matokeo ya vipimo hivyo yalitarajiwa kutolewa leo Jumanne.
Ikumbukwe pia kuwa, rais huyo wa Brazil amekuwa akijifananisha sana rais wa Marekani, Donald Trump na mwezi Aprili mwaka huu, alikataa kuchukua hatua za kitaifa za kukabiliana na maambukizi ya kirusi cha corona. Matokeo yake ni kwamba hivi sasa baada ya Marekani, Brazil ndiyo nchi yenye wagonjwa na vifo vingi zaidi vya wagonjwa wa COVID-19 duniani.
Maambukizi ya corona yameenea katika kona zote za Brazil. Hivi sasa zaidi ya watu milioni moja na laki sita na 27 elfu wameambukizwa kirusi hicho nchini humo na zaidi ya watu 66 elfu wameshafariki dunia.
Moja ya sababu kuu za kuenea kwa kasi na kwa kiwango kikubwa ugonjwa wa COVID-19 nchini Brazil ni misimamo ya rais wa nchi hiyo ambaye ni maarufu kwa jina la Trump wa Brazil. Rais huyo analaumiwa kwa kudai kuwa ugonjwa wa corona ni ugonjwa mdogo tu wa mafua na kwa kupinga kuchukua hatua za maana za afya kama vile karantini na uchungaji wa masafa baina ya watu ili kukabiliana na corona.
342/