10 Julai 2020 - 09:40
Hashtagi ya "Masharifu Wawili, Nembo ya Heshima Yetu" yaanzishwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Iraq

Watumiaji wa mitandao ya kijamii katika nchi za Iran na Iraq wameanzisha kampeni kwenye mitandao hiyo, ya hashtagi ya #Masharifu Wawili _ Ali Wawili _ Nembo ya Heshima Yetu, wakisisitizia umoja na mshikamano wa nchi mbili katika kukabiliana na maadui.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kanali ya televisheni ya al-Alam imeripoti kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii katika nchi za Iran na Iraq wamesambaza Hashtagi hiyo ya "Masharifu Wawili, Ali Wawili, Nembo ya Heshima Yetu" inayoashiria majina ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Ayatullah Sayyid Ali Sistani, Marjaa Taqlidi wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq na kutangaza kuwa, mifumo ya kiistikbari haitaweza katu kuzusha mfarakano baina ya mataifa mawili ya Iran na Iraq ambayo yalikuwa bega kwa bega katika medani za vita dhidi ya kundi la kigaidi ya DAESH (ISIS).

Watumiaji hao wa mitandao ya kijamii wamelaani pia hatua ovu na chafu ya gazeti la Kisaudi la ash-Sharqul-Awsat dhidi ya Ayatullah Sistani na kueleza kwamba: Ayatullah Sistani na Ayatullah Khamenei wanachukua mwafaka za kuzima njama za maadui; na ndio maana Marekani, utawala wa Kizayuni na waitifaki wao wanaelekeza hujuma zao kwa viongozi wa juu wa kidini wa Kishia.

Itakumbukwa kuwa Ijumaa ya wiki iliyopita, gazeti la Kisaudi la ash-Sharqul-Awsat lilichapisha katuni ya kumvunjia heshima Ayatullah Sistani, kiongozi wa juu wa kidini anayeheshimika mno, wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, kitendo ambacho kiliamsha wimbi la ghadhabu na radiamali kali za kuulaani utawala wa Aal Saud na vyombo vyake vya habari.../

342/