Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Muswada uliokuwa umependekezwa na Marekani kwa ajili ya kuongeza muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umeshindwa vibaya baada ya kupigiwa kura mbili za kuupinga, mbili za kuukubali huku wanachama 11 wakijizuia kupiga kura.
Ni Marekani na Jamhuri ya Dominican pekee ndizo zilizoupigia muswada huo kura ya ndio. China na Russia zimeupinga baada ya kupiga kura ya hapana huku wanachama wengine wakijizuia kupiga kura; na hivyo kuifanya Marekani ishindwe vibaya.
Marekani imeshindwa vibaya licha ya kuufanyia marekebisho kadhaa muswada wake huo Jumanne iliyopita baada ya kutambua kwamba, hautapata kura zinazohitajika. Licha ya marekebisho hayo yaliyolenga kuzishawishi baadhii ya nchi wanachama ziafikiane nayo, lakini hatua hiyo nayo haijawa na mafanikiio.
Kwa muuktadha huo, kama ilivyokuwa iimekubaliwa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Iran itaondolewa vikwazo vya silaha ifikapo tarehe 18 Oktoba mwaka huu.
Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ambaye amekasirishwa mno na kugonga ukuta mpango wa nchi yake amenukuliwa akisema kuwa, Washington itaendelea na juhudi zake. Kufeli mpango huo ni ujumbe wa wazi kwamba, walimwengu wamechoshwa na siasa za kibabe na za utumiaji mabavu za Marekani.
342/