Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Balozi wa Marekani katika utawala wa Kizayuni wa Israel David D. Friedman amesema katika mahojiano na gazeti la Israel Hayom kwamba, serikali ya Washington imekusudia kumbadilisha kwa kumuondoa uongozini Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
Kufuatia kutolewa matamshi hayo na Friedman dhidi ya Abbas, Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mohammad Shtayyeh amesema, serikali ya Marekani itakuwa inaota kama inadhani kwamba inaweza kuwatwisha Wapalestina matakwa yake.
Shtayyeh amesisitiza kuwa: Msimamo thabiti na ushujaa wa Mahmoud Abbas katika kutetea haki za watu wa Palestina umewaghadhibisha viongozi wa Marekani na wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Hivi karibuni Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniya walisisitiza katika mazungumzo waliyofanya kwa njia ya simu kuwa makundi yote ya Palestina yamejipanga kwenye ngome na safu moja, na yameungana ili kuchukua hatua kwa pamoja za kukabiliana na njama za maadui dhidi ya Palestina.
Msimamo huo umetangazwa kufuatia hatua ya kiuhaini na ya usaliti iliyochukuliwa na Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Makundi na mirengo yote ya Palestina imelaani na kupinga hatua hiyo yakisisitiza kuwa ni sawa na kuyachoma jambia la mgongo malengo matukufu ya Palestina.../
342/