Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:Rais Rouhani ameyasema hayo Jumatatu mjini Tehran katika mkutano na watu wenye kutoa misaada na mashirika yasiyo ya kiserikali na kuongeza kuwa: "Taifa la Iran halikulegeza msimamo mbele ya mashinikizo ya juu kabisa ya adui na limesimama kidete." Amesema hivi sasa hakuna nchi isiyokiri kuwa Iran imeipa Marekani pigo la kistratijia.
Rais wa Iran ameendelea kusema kuwa, wakuu wa sasa wa Marekani na hata wa serikali iliyopita wanakiri kuwa mashinikizo yao dhidi ya Iran hayakufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha Rais wa Iran amebainisha kuwa, Marekani ilikuwa inalenga kuhakikisha kuwa kwa mashinikizo yake ya juu, Iran ingesalimu amri kwa muda wa miezi sita au mwaka mmoja lakini haikufanikisha lengo hilo.
Rouhani pia amesema hakuna yeyeote aliyeisaidia Iran na hata wakati wa janga la corona, adui aliendeleza mashinikizo yake dhidi ya Iran.
Rais wa Iran ameongeza kuwa: "Wimbi la nne la corona ambalo tunakabiliana nalo haliwezi kulinganishwa na mawimbi yaliyotangulia na si tu Iran bali nchi zingine za dunia zinakabiliana na wimbi hilo."
Rais Rouhani amessema pamoja na hali hiyo, wananchi wa Iran watasaidiana katika kukabiliana na hali iliyoibuka.
342/