Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ndagijimana amesema kuwa uchumi wa Rwanda unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.1 katika mwaka 2021, asilimia 7 katika mwaka 2022 na asilimia 7.8 katika mwaka 2023 na mwaka 2024.
Waziri Ndagijimana amesema ustawi huo wa kiuchumi mwaka huu unatokana na udhibiti wenye ufanisi wa janga la COVID-19 nchini humo.
Aidha amesema, Rwanda imepata maendeleo makubwa katika kuboresha mazingira yake ya uwekezaji, na itaendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa mujibu wa mkakati wa mageuzi ya taifa na mpango wa maendeleo wa mwaka 2050, ili kuunga mkono uwekezaji wa ndani na wa kimataifa.
Hivi sasa Rwanda inatekeleza mpango wa kuwa kitovu cha kimataifa cha kifedha na iko mbioni kuwavutia wawekezaji wapya katika sekta ya masoko ya kifedha.
Uchumi wa Rwanda ulidorora kwa asilimia 2.3 mwaka wa kifedha wa 2019-2020 baada ya kustawi kwa asilimia 8.8 mwaka uliotangulia. Uchumi wa nchi hiyo ulidorara kutokana na janga la COVID-19 ambalo lilitoa pigo kubwa kwa harakati za kiuchumi katika nchi hiyo.
342/