29 Agosti 2021 - 11:17
Amir-Abdolanian: Iran inaunga mkono usalama, mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi ya Iraq

Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inaunga mkono usalama, mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi ya Iraq.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hussein Amir-Abdolahian, Waziri mpya wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo katika mkutano unaofanyika Baghdad wa himaya ya kieneo kwa Iraq na kubainisha kwamba, Iraq mpya ya sasa inahitajia ukarabati na kuboresha mahusiano ya kieneo na kwamba, mahudhurio ya nchi za eneo katika mkutano huo ni ishara ya wazi ya kuweko jitihada za nchi hiyo za kuandaa mazingira mwafaka ya kupatikana ushirikiano baina ya mataifa ya eneo hili la Asia Magharibi.

Amir-Abdolahian ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kuunga mkono amani, usalama, uthabiti, mamalaka ya kujitawala, umoja wa ardhi yote ya Iraq, izza, heshima na kuboreshwa nafasi ya kieneo na kimataifa ya nchi hjiyo, inatangaza wazi utayari wake wa kupanua ushirikiano wa pande mbili na wa kieneo.

342/