Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Vladimir Putin wa Russia amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la TASS alipokuwa akizungumza katika kikao cha wazi cha Jukwaa la Uchumi la Mashariki kinachoendelea huko Vladivostok, kusini mashariki mwa Russia.
Amefafanua kwa kusema: Kuhusu Iran, taifa hilo linahitaji msaada lakini mpaka sasa hakuna vizuizi vilivyoondolewa. Hakuna hata mazungumzo yanayoendelea juu ya suala hili.
Putin amebainisha kuwa, masuala ya kisiasa hayapaswi kuoanishwa na masuala ya kibinadamu na kwamba kuna udharura wa kuondolewa vizingiti Iran ili ipige hatua katika vita dhidi ya janga la Corona.
Rais wa Russia ameeleza bayana kuwa, nchi za Magharibi ambazo zinajidai kuwa vinara wa haki za binadamu duniani, zimepuuza kabisa suala la kuliondolea taifa la Iran vikwazo vikiwemo vile vinavyohusiana na uagizaji wa dawa na chanjo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran, idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa COVID-19 hapa nchini kufikia jana Ijumaa ni 109, 549, huku idadi ya kesi za maradhi hayo zilizonakiliwa kufikia sasa ikipindukia milioni tano.
342/